BLACK STONE YABEBA UBINGWA - LIGI YA PIKIPIKI KIMAMBA.



Kikosi cha BLACK STONE

NA COSMAS DOSSANTOS
MOROGORO.


Klabu ya BLACKSTONE imewapa burudani ya nafsi mashabiki wake leo Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KIMAMBA FIBRES katika mchezo wa hatua ya fainali ya ligi ya Pikipiki aina ya SANLG katika Uwanja wa Kimamba Secondary School maarufu kama Mabatini Studium.

Mpira ulianza kwa kasi baada ya timu hizo zote mbili kushambuliana kwa vipindi mpaka dakika ya 35 katika kipindi hicho cha kwanza lakini katika dakika ya 37 BLACKSTONE walionekana kuchangamka zaidi na kuonyesha kwa mashabiki wake kuwa wanatafuta kitu.

Kikosi cha KIMAMBA FIBRES

Katika kipindi hicho cha kwanza dakika ya 39 Mshambuliaji DULLA ZUNGU aliweza kuwanyanyua mashabiki na wapenzi wa BLACKSTONE kwa kufunga goli maridadi kabisa bila presha ya kusongwasongwa na walinzi wa KIMAMBA FIBRES baada ya mlinzi wa kati wa Timu hiyo AMIRI CHUMVI kufanya kosa la kuupiga mpira kichwa ambao haukwenda mbali ndipo Mshambuliaji wa BACKSTONE akaweza kuutendea haki mpira huo na kuuweka kimiyani.

Mpaka timu hizo zinakwenda mapumziko matokeo yalikuwa BLACKSTONE anaongoza moja kwa  bila dhidi ya KIMAMBA FIBRES.

Mshambuliaji DULLA ZUNGU  wa BLACKSTONE

Hivyo bao hilo la pekee lilolofunga na mshambuliaji DULLA ZUNGU  limewafanya BLACKSTONE kuwa mabingwa wa Ligi hiyo ya Pikipiki aina ya (SANLG) kwa mwaka 2017 katika Wilaya ya Kilosa, Tarafa ya Kimamba Mkoani Morogoro.

Na baada timu hizo kurudi uwanjani hali ya mchezo ilibadilika zaidi baada ya wachezaji wa KIMAMBA FIBRES kuonekana kupambana zaidi ili kutafuta goli la kusawazisha katika kipindi hicho cha pili. Lakini jitihada za timu hiyo zilionekana kugonga mwamba kwa safu ya Ulinzi ya BLACKSTONE kuwa makini zaidi na kukaba kwa kushirikiana tena kwa umoja wa hali ya juu .

Kawaida ya mchezo wa mpira wa miguu huwa ni dakika 90, Mpaka mwamuzi wa mchezo huo anapuliza kipyanga hicho kuashiria mchezo umemalizika matokeo yalikuwa BLACKSTONE 1-0 KIMAMBA FIBRES.
BLACK STONE YABEBA UBINGWA - LIGI YA PIKIPIKI KIMAMBA. BLACK STONE YABEBA UBINGWA  - LIGI YA PIKIPIKI KIMAMBA. Reviewed by Abdurazak Ngowo on September 22, 2017 Rating: 5

No comments:

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
Powered by Blogger.