MANCHESTER UNITED NDIO KINARA WA MAPATO KWA VILABU DUNIANI.

Mauzo makubwa ya jezi ni moja ya chanzo cha mapato kwa United

Timu ya Manchester United imepata kipato kikubwa kuliko timu yoyote katika msimu uliopita kulingana na taarifa zilizochapishwa na kampuni kubwa ya ukaguzi duniani (Deloitte).
Manchester United imewashinda Real Madrid waliofanya vizuri katika michezo kwa miaka 11baaada ya kukusanya kipato kikubwa takribani Euro 689 katika msimu wa 2015-2016.
Clubu za ligi ya Premier imeshuhudia kukua kwa kipato kwa Euro Millioni mia moja.
Ukijumlisha vipato vya timu ishirini bora kwa msimu wa 2015-2016 vimeongezeka kwa asilimia 12% na kufikia euro billioni 7.4 hii haijawahi kutokea.
Hii ni mara ya kwanza kwa Man U kushikilia nafasi hiyo tokea msimu wa 2003-04.
Real Madrid wameshuka mpaka nafasi ya tatu wakiwaacha wapinzani wao wakubwa Barcelona katika nafasi ya pili.

Madrid imeshuka mpaka nafasi ya tatu

Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wapo nafasi ya nne huku matajiri wa jiji la Manchester Man City wakiwa nafasi ya tano kwa kutengeneza Euro milioni524 kwa msimu uliopita.
Hii ni mara ya kwanza kwa city kuingia katika nafasi hiyo.

Msimamo kwa Mapato Orodha ya Deloitte 2015-16
Klabu (Nafasi msimu uliopita) Mapato kwa €m (£m kwenye mabano) 2015-16 Mapato 2014-15
1 (3) Manchester United 689 (515.3) 519.5 (395.2)
2 (2) Barcelona 620.2 (463.8) 560.8 (426.6)
3 (1) Real Madrid 620.1 (463.8) 577 (439)
4 (5) Bayern Munich 592 (442.7) 474 (360.6)
5 (6) Manchester City 524.9 (392.6) 463.5 (352.6)
6 (4) Paris St-Germain 520.9 (389.6) 480.8 (365.8)
7 (7) Arsenal 468.5 (350.4) 435.5 (331.3)
8 (8) Chelsea 447.4 (334.6) 420 (319.5)
9 (9) Liverpool 403.8 (302) 391.8 (298.1)
10 (10) Juventus 341.1 (255.1) 323.9 (246.4)
MANCHESTER UNITED NDIO KINARA WA MAPATO KWA VILABU DUNIANI. MANCHESTER UNITED NDIO KINARA WA MAPATO KWA VILABU DUNIANI. Reviewed by Abdurazak Ngowo on January 19, 2017 Rating: 5

No comments:

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
Powered by Blogger.