JE! NI TIMU GANI KUTOKA KIFUAMBELE JUMAPILI HII.

MANCHESTER UNITED vs LIVERPOOL
Mbio za kugombania ubingwa wa Kombe la Premier League sasa zimeshika hatamu na joto limepanda kwa mahasimu wawili Manchester United na Liverpool ambao watachuana vikali pale Old Trafford Jumapili ya wiki hii. Liverpool wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya Uingereza mpaka sasa nyuma ya vinara Chelsea na wanaingia kwenye mechi hii wakiwa vifua mbele, lakini United nao wanaweza kupunguza tofauti ya pointi iliyopo mpaka kubakisha mbili tu endapo watapata ushindi katika mtanange huu.

Kazi iliyokuwa ikiotewa ndoto na Jose Mourinho ya kuinoa na kuiongoza Manchester united imegeuka kuwa ujinamizi baada ya kuanza kwa kusuasua na kuambulia suluhu tatu mfululizo mwezi Desemba, lakini ushindi mara sita mfululizo walioupata hivi karibuni umewafanya Mashetani hawa wekundu kupata matumaini ya kumaliza ligi ndani ya nafasi nne za juu msimu huu na huenda ikawa Zaidi ya matumaini haya kwa kumaliza nafasi nzuri Zaidi.

Pande zote zimeshiriki mechi za kuwania Kombe la EFL hatua ya nusu fainali kabla hawajakutana pale Old Trafford lakini Klopp na Mourinho wote tayari watakuwa wameelekeza hisia zao katika mchezo huu ambao hakika utakuwa ni wa kusisimua na kukata na shoka mjini Salford!

JE! NI TIMU GANI KUTOKA KIFUAMBELE JUMAPILI HII. JE! NI TIMU GANI KUTOKA KIFUAMBELE JUMAPILI HII. Reviewed by Abdurazak Ngowo on January 13, 2017 Rating: 5

No comments:

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
Powered by Blogger.